• HABARI MPYA

  Thursday, August 04, 2016

  SAMATTA AZIDI KUPASUA MAWIMBI EUROPA LEAGUE, ATINGA MCHUJO WA MWISHO

  Na Mwandishi Wetu, CORK
  NAHODHA wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta amecheza vizuri usiku huu, KRC Genk ikishinda ugenini 2-1 dhidi ya Cork City FC ya Ireland na kufuzu hatua ya mwisho ya mchujo kuwania kucheza hatua makundi ya Europa League wakati.
  Ushindi wa leo Uwanja wa Turner's Cross, mjini Cork, Ireland unafanya Genk isonge mbele kwa ushindi wa jumla wa 3-1, baada ya wiki iliyopita kushinda 1-0 mjini Genk.
  Mabao ya Genk leo yamefungwa na Thomas Buffel dakika ya 12 na Sebastien Dewaest dakika ya 41, wakati la wenyeji lilifungwa na Alan Bennett dakika ya 63.

  Na Samatta aliyewekewa ulinzi mkali na mabeki wa Cork City FC, alicheza kwa dakika 77 kabla ya kumpisha Bryan Heynen kumalizia mechi hiyo.
  Droo ya hatua ya mwisho ya mchujo inatarajiwa kupangwa kesho (Agosti 5, 2016) na mechi za kwanza zitachezwa Agosti 18 wakati marudiano yatakuwa Agosti 25.
  Vikosi vilikuwa, Cork City FC: McNulty, Bennett, Bolger, Beattie, Dooley, O'Connor, Gearoid Morrissey/Danny Morrissey, McSweeney/45 'O'Sullivan, Browne, Maguire/Sheppard dk54 na Buckley.
  KRC Genk : Bizot, Walsh, Dewaest Wouters, Uronen, Ndidi, Pozuelo, Bailey/Trossard dk65, Buffalo/Tshimanga dk83, Kebano na Samatta/Heynen dk77.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SAMATTA AZIDI KUPASUA MAWIMBI EUROPA LEAGUE, ATINGA MCHUJO WA MWISHO Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top