• HABARI MPYA

    Friday, August 05, 2016

    RONALDO APEWA BALE NA GRIEZMANN TUZO YA MWANASOKA BORA ULAYA

    NYOTA wawili wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo na Gareth Bale watapambana na Antoine Griezmann wa Atletico Madrid kuwania tuzo ya Mwanasoka Bora wa Mwaka wa Ulaya.
    Bodi ya Soka Ulaya (UEFA) imetangaza orodha fupi ya mwisho ya wachezaji watatu wa kuwania tuzo hiyo leo na wachezaji wa la Liga watupu watachuana, tena wote kutoka timu za Jiji la Madrid.
    Mshindi wa tuzo hiyo atapatikana baada ya kupigiwa kura na matokeo yatatangazwa katika Grimaldi Forum mjini Monaco Agousti 25.
    Waandishi wa Habari kutoka nchi zote wanachama 55 wa UEFA watawasilisha orodha yao fupi, huku 54 wakipiga kura.

    Cristiano Ronaldo anapewa nafasi kubwa ya kubeba tuzo ya Mwanasoka Bora wa Ulaya Agosti 25, mwaka huu PICHA ZAIDI GONGA HAPA 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: RONALDO APEWA BALE NA GRIEZMANN TUZO YA MWANASOKA BORA ULAYA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top