• HABARI MPYA

  Tuesday, August 02, 2016

  MANJI AITISHA MKUTANO WA DHARULA YANGA BAADA YA DEWJI KUKUBALIWA KUINUNUA SIMBA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MWENYEKITI wa Yanga SC, Yussuf Manji ameitisha Mkutano wa dharula wa wanachama utakaofanyika Jumamosi wiki hii ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam.
  Manji anaitisha Mkutano huo siku mbili tu baada ya wapinzani, Simba SC kuamua kuingia katika mfumo wa kuuza hisa kufuatia Mkutano wao wa Jumapili ukumbi wa Bwalo la Maofisa wa Polisi, Oysterbay, Dar es Salaam.
  Barua ya tangazo la Mkutano wa Yanga haijataja agenda – na Mkutano huo unakuja miezi miwili tu tangu kufanyika kwa uchaguzi Mkuu Juni 11, mwaka huu.
  Manji (kushoto) akijadiliana na Makamu wake Mwenyekiti, Clement Sanga
  Simba imekubali mabadiliko kutoka klabu kuwa mali ya wanachama wote na kuamua kuuza hisa – na tayari bilionea Mohamed Dewji ametoa ofa ya kununua asilimia 51 ya hisa za klabu kwa Sh. Bilioni 20.
  Wakati huo huo: Yanga SC itakuwa na mchezo wa kirafiki Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam dhidi ya Mtibwa Sugar ya Morogoro, yakiwa ni maandaliai ya mchezo wao wa Kundi A Kombe la Shirikisho Afrika wiki ijayo dhidi ya MO Bejaia ya Algeria.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MANJI AITISHA MKUTANO WA DHARULA YANGA BAADA YA DEWJI KUKUBALIWA KUINUNUA SIMBA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top