• HABARI MPYA

  Thursday, August 04, 2016

  AS KIGALI YASAJILI WAKALI WAWILI WA APR

  TIMU ya AS Kigali imefanikiwa kuwasajili wachezaji wawili wa APR, Nahodha Ismael Nshutiyamagara maarufu kama ‘Kodo’ na Tumaine ‘Tity’ Ntamuhanga kwa Mkataba wa miaka miwili kila mmoja.
  AS Kigali imethibitisha leo katika taarifa yake kwamba Kodo anayefahamika kwa uzoefu wake katika beki ya kati pamoja na uongozi mzuri kwa wachezaji wenzake, anatarajiwa kuongoza kampeni za klabh hiyo kushindania mataji msimu ujao.
  “Tulikosa kiongozi kwenye safu ya ulinzi na ushambuliaji, hivyo kuwasili kwa Kodo na Tity kunaleta uzoefu mwingi na uongozi katika timu yetu,” alisema kocha Mkuu wa AS Kigali, Eric Nshimiyimana.

  Ismael Nshutiyamagara amejiunga na AS Kigali kutoka APR, zote za Rwanda

  Wawili hao wanaungana na orodha ya wachezaji watatu walioondoka timu hiyo ya Jeshi kujiunga na timu ya Jiji la Kigali, wengine wakiwa ni washambuliaji Bernabe Mubumbyi na Michel Ndahinduka na kipa mkongwe, Jean Claude Ndoli.
  Klabu hizo zimefanya biashara kubwa dirisha hili la usajili, ikiwemo APR kumsajili mfungaji bora Muhadjiri Hakizimana kwa mkataba wa kudumu na mshambuliaji, Onesme Twizeyimana kwa mkopo kutoka  AS Kigali.
  AS Kigali ilimsajili Hakizimana kutoka Mukura Victory Sports mwezi uliopita, lakini ndani ya wiki moja baadaye, APR ikamsajili kutoka AS Kigali.
  AS Kigali pia imenunua huduma za Nahodha wa St Eloi Lupopo ya DRC, Kabange Twite, Alexis Nkomezi kutoka Sunrise FC na mshambuliaji Mganda, Karim Ndugwa wakiimarisha safu yao ya ushambuliaji kufuatia kuondoka kwa Ernest Sugira waliyemuuza AS Vita.
  AS Kigali ilimaliza katika nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi ya Rwanda msimu uliopita kwa pointi zake 56 wakizidiwa 11 na mabingwa, APR.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AS KIGALI YASAJILI WAKALI WAWILI WA APR Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top