• HABARI MPYA

  Saturday, July 16, 2016

  ZESCO YAJISAFISHIA NJIA NUSU FAINALI LIGI YA MABINGWA, YAITANDIKA 3-1 ASEC

  TIMU ya Zesco United ya Zambia imejiweka kwenye nafasi nzuri ya kwenda Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, kufuatia ushindi wa 3-1 nyumbani dhidi ya ASEC Mimosa ya Ivory Coast leo.
  Shukrani kwa, wafungaji wa mabao hayo, Jackson Mwanza, John Ching’andu na Idriss Mbombo katika mchezo huo wa mwisho wa mzunguko wa kwanza Kundi A uliofanyika Uwanja wa Levy Mwanawasa.
  Zesco United sasa inapanda nafasi ya pili kwenye kundi hilo baada ya kufikisha pointi sita sawa na vinara, Wydad Casablanca ya Morocco ambayo inacheza na Al Ahly usiku huu.
  Zesco inaweza kwenda Nusu Fainali iwapo iwapo itaepuka kufungwa na ASEC katika mchezo wa marudiano Julai 27 mjini Abidjan na pia kwenye mechi zake nyingine mbili zijazo dhidi ya Al Ahly ugenini na Wydad Casablanca nyumbani mwezi ujao.
  Mwanza alifunga dakika ya 32 hilo likiwa bao lake la kwanza kwenye mashindano haya na Ching’andu akafunga la pili na la tatu kwake kwenye mashindano haya na kuifanya Zesco iongoze 2-0 hadi mapumziko.
  Youssouf Dao aliyetokea benchi akaifungia bao la kwanza ASEC dakika ya 76, lakini dakika mbili baadaye Idriss Mbombo akaifungia bao la tatu Zesco baada ya kuingia kuchukua nafasi ya Mwanza dakika ya 68. Hilo linakuwa bao la tano kwa Mbombo kwenye mashindano haya.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ZESCO YAJISAFISHIA NJIA NUSU FAINALI LIGI YA MABINGWA, YAITANDIKA 3-1 ASEC Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top