• HABARI MPYA

  Saturday, July 16, 2016

  ZESCO NA ASEC NI PATASHIKA LA MAANA LEO LIGI YA MABINGWA

  TIMU ya Zesco United ya Zambia leo inaikaribisha Asec Mimosa ya Ivory Coast katika mchezo wa Kundi A Ligi ya Mabingwa Afrika.
  Zesco na ASEC zote kila moja ina pointi tatu baada ya kushinda mechi moja na kufungwa moja katika Raundi mbili za awali na kila moja itahitaji kushinda leo ili kufufua matumaini ya kwenda Nusu Fainali.
  Mchezo mwingine wa kundi hilo, Al Ahly ya Misri itakuwa mwenyeji wa vinara wa kundi, Wydad Casablanca ya Morocco. 
  Zesco United wanaikaribisha ASEC Mimosa leo Ligi ya Mabingwa

  MISIMAMO YA MAKUNDI LIGI YA MABINGWA AFRIKA

  Kundi A

  NaTimuPWDLGFGAGDPts
  1Wydad Casablanca22003036
  2ASEC Mimosas21012203
  3Zesco United210134-13
  4Al Ahly200235-20

  Kundi B

  NaTimuPWDLGFGAGDPts
  1Mamelodi Sundowns11002113
  2Zamalek11001013
  3Enyimba200213-20

  Wydad inaongoza kundi hilo kwa pointi zake sita, wakati Ahly haina pointi baada ya kufungwa mechi zote za mwanzo na inashika mkia kundini.
  Kundi B, Zamalek ya Misri kesho watakuwa wenyeji wa Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, wakati Enyimba watakuwa mapumzikoni.
  Ikumbukwe ES Setif ya Algeria iliondolewa kwenye mashindano hayo katika Kundi B baada ya vurugu za mashabiki wake.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ZESCO NA ASEC NI PATASHIKA LA MAANA LEO LIGI YA MABINGWA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top