• HABARI MPYA

  Wednesday, July 20, 2016

  YANGA WAIINGILIA KAMBINI MEDEAMA LEO DAR

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KIKOSI cha Yanga SC kinatarajiwa kuingia kambini leo katika hoteli ya Tiffany, katikati ya jiji la Dar es Salaam kuanza rasmi maandalizi ya mchezo wa marudiano wa Kundi A Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Medeama FC ya Ghana.
  Yanga watakuwa wageni wa Medeama Jumatano ya Julai 27, mwaka huu Uwanja wa Sekondi Sports au Essipong mjini Sekondi-Takoradi, Ghana katika mchezo huo wa kwanza wa marudiano mzunguko wa pili Kombe la Shirikisho, siku ambayo vinara wa kundi hilo, TP Mazembe wataikaribisha Mouloudia Olympique Bejaia mjini Lubumbashi.
  Timu hizo zitarudiana kiasi cha wiki baada ya kutoa sare katika mechi zao za kwanza, Yanhga 1-1 na Medema ana MO Bejaia 0-0 na Mazembe.
  Mazembe inaongoza Kundi A kwa pointi zake saba, ikifuatiwa na MO Bejaia pointi tano, Medeama pointi mbili, wakati Yanga yenye pointi moja inashika mkia.  
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA WAIINGILIA KAMBINI MEDEAMA LEO DAR Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top