• HABARI MPYA

    Friday, July 15, 2016

    TUZO ZA LIGI KUU 2016, NANI ATAMBWAGA NANI JUMAPILI?

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SAALAM
    SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limetangaza wanamichezo wote wanaowania tuzo 13 kwenye hafla ya washindi wa Ligi Kuu ya Vodacom kwa msimu wa 2015/2016 itakayofanyika Jumapili (Julai 17 mwaka huu) kwenye hoteli ya Double Tree by Hilton jijini Dar es Salaam.
    Aina 13 za tuzo ya Ligi hiyo inayodhaminiwa na kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania zitatolewa kwa washindi chini ya uratibu wa Kamati ya Tuzo ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) inayoundwa na waandishi wa habari za michezo, makocha, viongozi (administrators) na wawakilishi kutoka kwa wadhamini (Vodacom na Azam Tv).
    Tuzo hizo na kiasi cha fedha wanazopata washindi kwenye mabano ni; 
    Juma Abdul (kushoto) na Farid Mussa (kulia) wote wamo kwenye kinyang'anyiro cha tuzo 

    1. Bingwa (sh. 81,345,723) 
    2. Mshindi wa pili  (sh. 40,672,861)
    3. Mshindi wa tatu (sh. 29,052,044)
    4. Mshindi wa nne (sh. 23,241,635)

    5. Timu yenye Nidhamu Bora (sh. 17,228,820)
    *Zilizopendekezwa kuwania tuzo hiyo ni:
    - JKT Ruvu
    - Mgambo Shooting na
    - Mtibwa Sugar


    6. Mchezaji Bora wa Ligi (sh. 9,228,820)
    *Waliopendekezwa (nominees) kuwania tuzo hiyo ni:
    - Shiza Kichuya (Mtibwa Sugar)
    - Juma Abdul (Yanga) na
    - Mohamed Hussein (Simba)

    7. Mfungaji bora 
    Amissi Tambwe (sh. 5,742,940)

    8. Kipa Bora (sh. 5,742,940)
    *Waliopendekezwa (nominees) kuwania tuzo hiyo ni:
    - Aishi Manula (Azam),
    - Beno Kakolanya (Tanzania Prisons) na
    - Deogratius Munishi (Yanga)

    9. Mchezaji Bora wa Kigeni (sh. 5,742,940)

    - Donald Ngoma (Yanga)
    - Thabani Kamusoko (Yanga)
    - Vincent Agban (Simba)

    10.  Kocha Bora (sh. 8,000,000)
    *Waliopendekezwa (nominees) kuwania tuzo hiyo ni:
    - Hans Van Pluijm (Yanga)
    - Mecky Maxime (Mtibwa Sugar) na
    - Salum Mayanga (Tanzania Prisons)

    11.  Mwamuzi bora (sh. 5,742,940)
    *Waliopendekezwa (nominees) kuwania tuzo hiyo ni:
    - Anthony Kayombo
    - Ngole Mwangole
    - Rajab Mrope

    12. Mchezaji Bora Chipukizi (sh. 4,000,000

    *Waliopendekezwa (nominees) kuwania tuzo hiyo ni:
    - Farid Mussa (Azam)
    - Mohamed Hussein (Simba)
    - Mzamiru Yasin (Mtibwa Sugar) na
    - Shiza Kichuya (Mtibwa Sugar)

    13. Goli bora la msimu (sh. 3,000,000)
    *Kinyang'anyiro cha goli bora ni:
    - Ibrahim Ajib (magoli mawili ) na
    - Amisi Tambwe  (goli moja)
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TUZO ZA LIGI KUU 2016, NANI ATAMBWAGA NANI JUMAPILI? Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top