• HABARI MPYA

  Friday, July 15, 2016

  TFF YATOA UFAFANUZI KUHUSU STAND UNITED

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KAMATI ya Uchaguzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imesema kwamba Stand United Football Club, ndiyo jina sahihi na halali lililosajiliwa kwa Msajili wa Klabu na Vyama vya Michezo kwa ajili ya timu hiyo ya Shinyanga.
  Katika kikao chake cha Julai 13, 2016, Kamati ya Uchaguzi ya TFF imetoa msimamo kuhusu suala la Stand United baada ya kupitia vielelezo vyote na kujadiliana na wadau wa Stand United na kubaini bayana kwamba Stand United Football Club, ndiyo jina sahihi na halali lililosajiliwa kwa Msajili wa Klabu na Vyama vya Michezo.

  Uchaguzi uliofanyika hivi karibuni kwenye Klabu ya Stand United una sifa zote za kuitwa uchaguzi huru na wa haki kwa vile mchakato ulihusisha wanachama halali klabu hiyo.
  Wanachama wa Stand United ambao hawakushiriki uchaguzi ikiwa ni pamoja na wale waliokwenda kundi la kampuni wana uhalali wa kuendelea kuwa wanachama wa Stand United.
  Viongozi waliochaguliwa katika uchaguzi wa Stand United FC ni halali na ni ruksa kwao kuendesha ofisi na shughuli za Stand United kwa ujumla.
  TFF inatambua daftari la Wanachama wa Stand United lililoboreshwa kwa maelekezo ya TFF.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TFF YATOA UFAFANUZI KUHUSU STAND UNITED Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top