• HABARI MPYA

  Wednesday, July 20, 2016

  TFF YAILIMA FAINI NAMUNGO NA KUIPANDISHA DARAJA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KAMATI ya Mashindano ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), imeipiga faini ya Sh. 500,000, Klabu ya Namungo FC ya Lindi kwa kila mechi ambayo mchezaji Imani Vamwanga aliichezea timu hiyo akitumia jina la Emmanuel T. Mwanga katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL), kituo cha Morogoro 2015/2016.
  Katika kikao kilichoketi Julai 14, 2016 kujadilina, kupitia, malalamiko na taarifa za waamuzi na Kamisaa za mashindano ya RCL katika kituo cha Morogoro, kamati imebaini kwamba Namungo ilifanya udanganyifu wa jina la mchezaji kwa kumsajili na kumchezesha mchezaji Imani Vamwanga leseni Na. 930909003 ya usajili wa Ligi Daraja la Kwanza FDL msimu wa 2015/2016 klabu ya Kurugenzi Mafinga akitumia jina la Emmanuel T. Mwanga.
  Kamati imebaini hayo kupitia taarifa za usajili, ripoti za waamuzi na makamisaa kwa michezo ambayo mchezaji tajwa hapo juu amecheza katika Mashindano ya Ligi ya mkoa wa Lindi na Mashindano ya Ligi ya Daraja la Kwanza FDL msimu wa 2015/16. Namungo inaadhibiwa kwa mujibu wa Kanuni ya 39 (1) inayozungumza adhabu kwa klabu.
  Kamati ya Mashindano ya TFF imetoa uamuzi huo kwa Namungo FC kupigwa faini ya Sh. 500,000 kwa kila mechi ambayo mchezaji Imani Vamwanga akitumia jina la Emmanuel T. Mwanga amecheza katika mashindano ya RCL.
  Pamoja na faini hiyo kwa kila mchezo ambao Namungo ilimchezesha mcheza huyo, timu hiyo Kamati ya Mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imeitangaza Namungo FC kupanda daraja kwenda Ligi Daraja la pili msimu wa 2016/2017 kama ilivyoainishwa kwenye kanuni ya 5 kipengere cha (4).
  Kamati imejiridhisha kwa kupitia taarifa za usajili, ripoti za waamuzi na makamisaa kwa michezo ambayo ilikuwa inalalamikiwa imefikia uamuzi huo kwa mujibu wa kanuni za mashindano hayo. Kamati imeipongeza na kukutakia kila la heri katika michezo.
  Wakati huo huo: TFF inaipongeza Klabu ya Pepsi FC ya Arusha kwa kupata nafasi ya kupanda daraja na kuingia Daraja la Pili SDL msimu wa 2016/2017 kwa mujibu wa kanuni ya 5 kipengele cha (5) ya mashindano ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa RCL msimu wa 2015/2016.
  Timu imefanikiwa kupata nafasi ya pili katika msimamo wa ligi ya mabingwa wa Mikoa 2015/2016 kituo cha Singida na kuongoza kati ya timu zilizoshika nafasi ya pili katika vituo vilivyosalia ambavyo ni Njombe, Morogoro na Muleba. TFF inaItakia kila la kheri katika maandalizi ya kushiriki Daraja la Pili msimu wa 2016/2017.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TFF YAILIMA FAINI NAMUNGO NA KUIPANDISHA DARAJA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top