• HABARI MPYA

  Saturday, July 16, 2016

  TAMBWE, CHIRWA NA NGOMA WAANZISHWA PAMOJA DHIDI YA MEDEAMA LEO TAIFA

  Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
  KOCHA Mholanzi wa Yanga, Hans van der Pluijm amewaanzisha pamoja Mzimbabwe, Donald Ngoma, Mrundi Amissi Tambwe na Mzambia Obrey Chirwa katika safu ya ushambuliaji kwa ajili ya mchezo dhidi ya Medeama FC. 
  Yanga inawakaribisha Medeama FC ya Ghana jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mchezo wa Kundi A Kombe la Shirikisho Afrika.
  Na Pluijm amerudia karibu kikosi chake kile kile kilochompa ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, langoni akimuweka Deogratius Munishi ‘Dida’, mabeki; kulia Juma Abdul, kushoto, Oscar Joshua na katikati Kelvin Yondani na Mtogot Vincent Bossou.
  Donald Ngoma ameanzishwa pamoja na Tambwe na Chirwa leo dhidi ya Medeama  

  Viungo ni Mbuyu Twite na Thabani Kamusoko katikati, wakati pembeni ni Simon Msuva na Chirwa na washambuliaji ni Tambwe na Ngoma.
  Wachezaji wa akiba ni Ally Mustafa ‘Barthez’, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Said Makapu, Haruna Niyonzima, Juma Mahadhi, Malimi Busungu na Andrew Vincent.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TAMBWE, CHIRWA NA NGOMA WAANZISHWA PAMOJA DHIDI YA MEDEAMA LEO TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top