• HABARI MPYA

  Tuesday, July 19, 2016

  STRAIKA LA LUPOPO LATUA SIMBA KUCHUKUA NAFASI YA MAVUGO

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MSHAMBULIAJI Masoud Cedrick Masanga amewasili kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na kujiunga na Simba SC ya Tanzania kwa majaribio.
  Masanga kutoka St Eloi Lupopo FC ya Lubumbashi, aliwasili juzi siku akiwa ameongozana na mchezaji mwingine, kiungo Sanga Bahende kutoka timu hiyo na moja kwa moja kwenda Morogoro ambako Simba imeweka kambi.
  Sasa kocha Mcameroon, Joseph Marius Omog atawaangalia wachezaji hao mazoezini kabla ya kutoa majibu kama wasajiliwe au la.
  Kocha Mcameroon wa Simba, Joseph Omog ameendelea kupokea wachezaji wapya wa majaribio Morogoro 
  Na Simba imewaleta wachezaji hao baada ya Mrundi Laudit Mavugo inayemtaka kudaiwa kutimkia Ufaransa kufanya mipango ya kujiunga na klabu ya Tours ya Ligi Daraja la Pili, maarufu kama Ligue 2.
  Mavugo amekwenda Ufaransa wakati tayari Simba SC wamesema wamekwishaingia Mkataba na mchezaji huyo kuanza kuwatumikia kuanzia msimu ujao.
  Bado haijulikani Simba SC itachukua gani kwa Mavugo, kwa kuwa makubaliano yao na mchezaji huyo bado yanafanywa siri ili kuepuka vikwazo kutoka klabu yake, Vital'O.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: STRAIKA LA LUPOPO LATUA SIMBA KUCHUKUA NAFASI YA MAVUGO Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top