• HABARI MPYA

  Tuesday, July 19, 2016

  SIMBA NA YANGA OKTOBA 1 TAIFA, RATIBA KAMILI LIGI KUU HII HAPA

  WATANI wa jadi, Simba na Yanga watakutana Oktoba 1, 2016 katika mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Kwa mujibu wa Ratiba ya Ligi Kuu iliyotolewa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) leo, michuano hiyo itaanza Agosti 20 kwa mechi saba kuchezwa kwenye viwanja tofauti, ikitanguliwa na mchezo wa Ngao ya Jamii kati ya Azam na Yanga Agosti 17, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Mechi za ufunguzi za Ligi Kuu Agosti 20, Simba SC watacheza na Ndanda FC Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, huku Azam wakiikaribisha African Lyon Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.

  Kagera Sugar wataanza na Mbeya City Uwanja wa Kaitaba, Bukoba, Toto Africans na Mwadui FC Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza, Stand United na Mbao FC Uwanja wa Kambarage, Shinyanga, Mtibwa Sugar na Ruvu Shooting Uwanja wa Manungu, Turiani, Morogoro na Majimaji na Prisons Uwanja wa Majimaji Songea.  
  Mabingwa watetezi, Yanga SC wataanza kutetea taji lao Agosti 31 dhidi ya JKT Ruvu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Na hiyo ni kwa sababu TFF imewapa nafasi ya kujiandaa na mchezo wao wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya TP Mazembe utakaochgezwa Agosti 23 mjini Lubumbashi, DRC.   RATIBA KAMILI YA LIGI KUU GONGA HAPA 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA NA YANGA OKTOBA 1 TAIFA, RATIBA KAMILI LIGI KUU HII HAPA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top