• HABARI MPYA

    Thursday, July 14, 2016

    RONALDO SASA NDIYE MWANAMICHEZO TAJIRI ZAIDI DUNIANI, MESSI TUPWA HUKO!


    Chris Brunskill Ltd/Getty Images 
    NYOTA wa Real Madrid na Ureno, Cristiano Ronaldo sasa ni kati ya wanamichezo wanne wanaoongoza kwa kuingiza fedha duniani, wakizidiwa tu mwanamuziki Taylor Swift, Boyband One Direction na James Patterson.
    Hiyo ni kwa mujibu wa taarifa za jarida la Forbes ambalo limesema mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 anaingiza kiasi cha dola za Kimarekani Milioni 88 kwa msimu. 
    Kiasi hicho kinamuweka juu ya mpinzani wake mkubwa, Lionel Messi wa Barcelona anayeingiza dola Milioni 81.5 katika nafasi ya pili na nyota wa timu ya mpira wa kikapu ya Cleveland Cavaliers, LeBron James anayeingiza dola Milioni 77 katika nafasi ya tatu.
    Orodha kamili ya wanamichezo 10 wanaoongozwa kulipwa kwa mujibu wa Forbes ni hii:
    Wanamichezo 10 wanaolipwa zaidi kwa mujibu wa Forbes
    NambaMuhusikaPato lake
    1.Taylor SwiftDola Milioni 170
    2.One DirectionDola Milioni 110 
    3.James PattersonDola Milioni 95
    =4.Cristiano RonaldoDola Milioni 88
    =4.Dr. Phil McGrawDola Milioni 88
    6.Kevin HartDola Milioni 87.5
    7.Howard SternDola Milioni 85
    8.Lionel MessiDola Milioni 81.5
    9.AdeleDola Milioni 80.5
    10.Rush LimbaughDola Milioni 79

    Kwa mujibu wa Forbes, Ronaldo anapata Dola Milioni 55 kutokana na mshahara tu, wakati fedha nyingine zinatokana na mikataba yake ya udhamini. 
    Mchezaji huyo wa zamani wa Manchester United anafanya kazi na makampuni ya Nike, TAG Heuer, Sacoor Brothers Suits na Monster.
    Si ajabu Mreno huyo kuongoza sasa kwa kipato hivi sasa, ikiwa hata uwanjani ameendelea kufanya vizuri na mwaka huu ukiingia katika moja ya miaka ya kukumb ukwa kwenye maisha yake ya soka.

    Shaun Botterill/Getty Images
    Huu ni mwaka wa kukumbukwa kwa Cristiano Ronaldo 
    Mei mwaka huu alifunga penalti ya ushindi dhidi ya mahasimu wao wa Jiji, Atletico Madrid katika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kabla ya wiki iliyopita kuiongoza Ureno kutwaa taji la Euro 2016 wakiwafunga wenyeji Ufaransa 1-0 katika fainali. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: RONALDO SASA NDIYE MWANAMICHEZO TAJIRI ZAIDI DUNIANI, MESSI TUPWA HUKO! Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top