• HABARI MPYA

  Saturday, July 16, 2016

  NGOLO KANTE ASAINI MIAKA MITANO CHELSEA NA KUSEMA; "NDOTO ZIMETIMIA"

  KIUNGO N'Golo Kante amesema kutua kwake Chelsea ni kutimia kwa ndoto zake baada ya kukamilisha uhamisho wa Pauni Milioni 30 kuhamia Stamford Bridge.
  Kante anajiunga na The Blues kwa Mkataba wa miaka mitano kutoka kwa mabingwa wa Ligi Kuu ya England, Leicester, ambako alitoa mchango mkubwa kwa The Foxes kutwaa taji hilo msimu uliopita. 
  Na kiungo huyo anasajiliwa Chelsea baada ya Michy Batshuayi kutoka Marseille.
  Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 alikaribia kusherehekea taji la pili mwaka 2016 baada ya timu yake ya taifa, Ufaransa kufungwa 1-0 na Ureno katika fainali ya Euro 2016. 

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NGOLO KANTE ASAINI MIAKA MITANO CHELSEA NA KUSEMA; "NDOTO ZIMETIMIA" Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top