• HABARI MPYA

  Thursday, July 14, 2016

  MESSI ANAVYOPUNGUZA 'STRESS' KWA PENZI LA ANTONELLA

  MWANASOKA bora wa dunia, Muargentina Lionel Messi ameendelea kujifariji na matatizo yanayomkabili kwa sasa kwa kujipumzisha na familia yake kabla ya kurejea Barcelona kwa maandalizi ya msimu mpya.
  Messi yuko na mkewe Antonella Roccuzzo na watoto mapumzikoni kwa sasa na picha zinaonyesha ni watu wenye furaha.
  Messi, amehukumiwa kifundo cha miaka miwili kwa kosa la kukwepa kodi Hispania na amestaafu soka ya kimataifa baada ya kushindwa kuisaidia Argentina kutwaa taji la Copa America.
  Yote hayo ameyaacha nyuma na kumchukua mkewe, Antonella na watoto wake wa kiune, Mateo na Thiago na kwenda kupumzika nao.

  Lionel Messi akipigwa busu na mkewe, Antonella Roccuzzo katika mapumziko yao  PICHA ZAIDI GONGA HAPA 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MESSI ANAVYOPUNGUZA 'STRESS' KWA PENZI LA ANTONELLA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top