• HABARI MPYA

  Wednesday, July 13, 2016

  LACINA TRAORE AENDA KUZIBA PENGO LA AHMED MUSA CSKA MOSCOW

  MABINGWA wa Urusi, CSKA Moscow wameimarisha safu ya ushambuliaji ya kikosi chao kwa kumsajili kwa mkopo wa muda mrefu mshambuliaji wa AS Monaco ya Ufaransa, Lacina Traore (pichani juu) leo.
  Mpachika mabao huyo mwenye umri wa miaka 25 raia wa Ivory Coast amefunga mabao manne katika mechi nane za kimataifa na anatarajiwa kuziba pengo la Ahmed Musa aliyejiunga na mabingwa wa England, Leicester City Ijumaa.
  Traore tayari amecheza Urusi kati ya mwaka 2011 na 2014 katika klabu za Kuban Krasnodar na Anji Makhachkala.
  Baada ya kujiunga na Monaco, alipelekwa kwa mkopo Everton ya England. Amefunga mabao matatu katika mechi 19 za Ligue 1 msimu uliopita.
  CSKA inatarajiwa kuuanza msimu mpya Julai 23 watakapomenyana na Zenit St. Petersburg kwenye mechi ya Super Cup na pia wamefuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: LACINA TRAORE AENDA KUZIBA PENGO LA AHMED MUSA CSKA MOSCOW Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top