• HABARI MPYA

  Friday, June 17, 2016

  ZAMALEK YABEBA 19 KUIFUATA ENYIMBA UFUNGUZI LIGI YA MABINGWA

  VIGOGO wa Misri, Zamalek wametangaza kikosi chao kitakachosafiri kwenda mjini Port-Harcourt, Nigeria kumenyana na wenyeji, Enyimba katika mchezo wa ufunguzi wa hatua ya makundi Ligi ya mMabingwa Afrika.
  Kocha Mkuu wa Zamalek, Mohammed Helmy amechukua wachezaji 19 kwa ajili ya mchezo huo wa Jumapili dhidi ya mabingwa mara mbili Afrika, akiwaacha Nahodha Mahmoud Shikabala na kiungo Ayman Hefny ambao wote hawako fiti.
  Kiungo Mnigeria, Moruf Yousef anapanda ndege kwenda Nigeria wakati mshambuliaji Mzambia, Emmanuel Mayuka yuko pia kwenye orodha.
  Enyimba na Zamalek wapo Kundi B katika Ligi ya Mabingwa Afrika sambamba na ES Setif ya Algeria na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.
  Kikosi kamili kinachopsafiri ni; Ahmed El-Shennawy, Mahmoud Genesh, Ali Gabr, Ahmed Dweidar, Hamada Tolba, Mohamed Adel Gomaa, Hazem Emam, Ramzy Khaled, Moruf Youssef, Ahmed Tawfik, Tarek Hamed, Ibrahim Abdel-Khalek, Mostafa Fathi, Mohamed Ibrahim, Mahmoud Kahraba, Bassem Morsy, Mohamed Salem, Ahmed Hassan Mekki na Emmanuel Mayuka.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ZAMALEK YABEBA 19 KUIFUATA ENYIMBA UFUNGUZI LIGI YA MABINGWA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top