• HABARI MPYA

  Monday, June 06, 2016

  YANGA YAMSAINISHA MIAKA MIAKA MIWILI KIPA WA PRISOSN ALIYEKUWA ANATAKIWA NA SIMBA

  Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
  KIPA wa Prisons ya Mbeya, leo Benno Kakolanya (pichani kulia) amesaini Mkataba wa miaka miwili kujiunga na wafalme wa soka ya Tanzania, Yanga SC.
  Usajili huo ni pigo kwa Simba SC ambao pia walikuwa wanamtaka kipa huyo, lakini ‘Chelewa Chelewa, mwana si wao tena” – kwani wenye kisu kikali wamefanya yao. 
  Akizungumza na BIN ZUBEIRY SPORTS – ONLINE leo, Kakolanya amesema kwamba amesaini Yanga baada ya kumaliza Mkataba wake wa miaka mitatu Prisons ya Mbeya.
  “Nimesaini miaka miwili kujiunga na Yanga, baada ya kumaliza Mkataba wangu Prsons,”amesema kakolanya ambaye ni kipa wa tatu wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars.
  Kakolanya sasa anakwenda kuungana na makipa watatu waliopo Yanga, Deo Munishi ‘Dida’, Ally Mustafa ‘Barthez’ na Benedicto Tinocco kufanya idadi ya makipa wanne.
  Hata hivyo, mustakabali wa Tinocco haueleweki sasa baada ya kusajiliwa kwa Kakolanya mwenye umri wa miaka 22, ambaye Prisons ilimuibua Mbaspo Academy.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA YAMSAINISHA MIAKA MIAKA MIWILI KIPA WA PRISOSN ALIYEKUWA ANATAKIWA NA SIMBA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top