• HABARI MPYA

  Tuesday, June 07, 2016

  YANGA SC YATAKA MILIONI 40 KUMUACHIA NONGA

  Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
  YANGA SC iko tayari kumuuza klabu yoyote anayotaka mshambuliaji Paul Nonga, iwapo litakapatikana dau la kuanzia Sh. Milioni 40.
  Nonga aliyejiunga na Yanga SC katika dirisha dogo Desemba kutoka Mwadui FC ya Shinyanga, ameuandikia barua uongozi wa klabu hiyo akiombwa kuachwa kwa sababu hapati nafasi ya kutosha ya kucheza.
  Na japokuwa bado Yanga hawajajibu barua hiyo ya Nonga, lakini wamekubaliana na kukubali kumuacha iwapo itatokea klabu ya kufidia gharama zilizotumika kumsajili Desemba.
  Paul Nonga (kushoto) akishangilia na Simon Msuva baada ya kufunga katika moja ya mechi 17 alizocheza Yanga tangu asajiliwe Desemba
  “Nonga alisajiliwa Desemba kwa gharama zaidi ya Sh. Milioni 30, na baada ya nusu msimu, anaomba kuachwa, sio anaomba kutolewa kwa mkopo, anaomba kuachwa,”.
  “Haina shida, sisi tutakuwa tayari kumuacha iwapo hiyo klabu inayomtaka itatulipa gharama zetu zisizopungua Sh. Milioni 40,”kimesema chanzo kutoka Yanga SC.
  Pamoja na kusajiliwa Desemba, Nonga amecheza mechi 17, Yanga SC nyingi akitokea benchi na kufanikiwa kufunga mabao sita katika mashindano yote.
  Nonga amemzidi idadi ya mechi za kucheza Matheo Anthony aliyesajiliwa mwanzoni mwa msimu uliopita kutoka KMKM ya Zanzibar, ambaye amecheza mechi 14 na kufunga mabao manne.
  Nonga amemzidi Matheo Anthony idadi ya mechi za kucheza Yanga SC

  Amemzidi pia kiungo mshambuliaji, Issoufou Boubacar kutoka Niger aliyecheza mechi 11 na kufunga mabao matatu, ambaye naye alisajiliwa mwanzoni mwa msimu.
  Na mechi alizocheza Nonga Yanga ndani ya nusu msimu, ni nusu ya idadi ya mechi za Malimi Busungu aliyesajiliwa mwanzoni mwa msimu hadi sasa akiwa amecheza mara 34 na kufunga mabao tisa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: YANGA SC YATAKA MILIONI 40 KUMUACHIA NONGA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top