• HABARI MPYA

    Friday, June 17, 2016

    UJERUMANI NGUVU SAWA NA POLAND, IRELAND YAIPIGA 2-0 UKRAINE EURO 2016

    Jerome Boateng (kulia) wa Ujerumani akipambana na mchezaji mwenzake wa Bayern Munich, Robert Lewandowski wa Poland katika mchezo wa Kundi C Euro 2016 uliomalizika kwa sare ya 0-0 Uwanja wa Stade de France mjini Paris, Ufaransa. Ujerumani sasa inaongoza kundi hilo kwa wastani wa mabao ikiwa na pointi nne sawa na Poland, wakati Ireland ya Kaskazini ni ya tatu kwa pointi zake tatu na Ukraine inashika mkia ikiwa haina pointi  PICHA ZAIDI GONGA HAPA 
    Wachezaji wa Ireland Kaskazini wakiwa wamemzingira mwenzao, Gareth McAuley baada ya kufunga bao katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Ukraine kwenye mchezo wa Kundi C Euro 2016 Uwanja wa Parc Olympique Lyonnais mjini Decines-Charpieu. Bao lingine la Ireland limefungwa na Niall McGinn  PICHA ZAIDI GONGA HAPA 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: UJERUMANI NGUVU SAWA NA POLAND, IRELAND YAIPIGA 2-0 UKRAINE EURO 2016 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top