• HABARI MPYA

  Saturday, June 04, 2016

  UGANDA WATANGULIZA MGUU MMOJA AFCON, WASHINDA 2-1 UGENINI

  TIMU ya taifa ya Uganda imeshinda 2-1 ugenini dhidi ya Botswana 2-1 katika mchezo wa Kundi D kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika jioni ye leo Uwanja wa Francistown Sports Complex mjini Francistown.
  Matokeo hayo yanaipeleka The Cranes kileleni mwa Kundi D, wakati Botswana inabaki nafasi ya tatu.
  Nahodha Geoffrey Massa alifunga bao dakika ya pili tu, lakini likakataliwa kwa madai alikuwa ameotea, lakini  dakika ya tisa Kizito Luwagga aliuwahi mpira mrefu wa Tony Mawejje na kumtungua kipa wa Botswana, Kabelo Dambe kuipatia Uganda bao la kwanza.

  kipa wa Cranes, Dennis Onyango alishindwa kumzuia Onkabetse Mankgatai kuisawazishia Botswana dakiak ya 50.
  Hata hivyo, sherehe za wenyeji hazikudumu sana baada ya Khalid Aucho kuifungia Uganda bao la pili dakika ya 53.
  Kikosi cha Botswana kilikuwa: Dambe, Gadibolae, Mafoko, Sosome, Ramoroka, Nato/Galenamotlhale dk36, Ditsele, Seakanyeng/Makgantai dk46, Moyana, Mogorosi na Ngele/Tshireletso dk73.
  Uganda: Onyango, Guma, Ochaya, Isinde, Junko, Wasswa, Khalid, Mawejje, Miya/Wasimbi dk65, Luwagga/Mugerwa dk89 na Massa/Okwi dk70.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: UGANDA WATANGULIZA MGUU MMOJA AFCON, WASHINDA 2-1 UGENINI Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top