• HABARI MPYA

  Sunday, June 05, 2016

  SIMBA NA AZAM ZAGOMBEA SAINI YA MGUNDA WA PRISONS

  Na Somoe Ng’itu, DAR ES SALAAM
  JINA la mshambuliaji wa Prisons ya Mbeya Jeremiah Juma Mgunda (pichani kulia) limo kwenye karatsati za timu zote mbili, Azam  na Simba za orodha ya wachezaji waliopendekezwa kusajiliwa kwa ajili ya ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
  Hata hivyo, kwa kuwa mchezaji huyo bado ana Mkataba na klabu yake, Prisons hakuna timu iliyofanya naye mazungumzo na zote sasa zinafikiria namna ya kuuingia uongozi wa Jeshi la Magereza nchini.
  Kwa kawaida limekuwa si jambo jepesi kutoa mchezaji mwenye Mkataba na timu za Majeshi – na mara nyingi wachezaji hupata misukosuko mizito haid ya kusweka rumande kwa kuondoka timu za taasisi hizo.
  Mgunda ni kati ya wachezaji waliong’ara katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu huu, akifunga mabao 11 nyuma ya Kipre Herman Tchetche wa Azam FC raia wa Ivory Coast.
  Mrundi Amissi Tambwe wa Yanga ndiye ameibuka kinara wa mabao msimu huu akifunga mara 21, akifuatiwa na Mganda Hamisi Kiiza mabao 19, Mzimbabwe Donald Dombo Ngoma na mzalendo Elias Maguri waliofunga mabao 14 kila mmoja.
  Na Mgunda katika soka anafuata nyayo za baba yake mzazi, Juma Mgunda aliyekuwa mshambuliaji hatari wa Coastal Union ya Tanga na timu ya taifa, Taifa Stars.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA NA AZAM ZAGOMBEA SAINI YA MGUNDA WA PRISONS Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top