• HABARI MPYA

    Tuesday, June 07, 2016

    PAZIA LA USAJILI LIGI KUU LAFUNGULIWA WIKI IJAYO

    Na Princess Asia, DAR ES SALAAM
    SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF), limesema kwamba zoezi rasmi la usajili wa wachezaji wa msimu ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara litaanza Juni 15, mwaka huu baada ya mapumziko ya wachazaji yanayoishia Juni 10, 2016.
    Kwa mujibu wa kalenda ya mwaka ya TFF, uhamisho wa wachezaji ambako utaanza Juni 15, 2016 hadi Julai 30, 2016.
    Kwa mujibu wa Kalenda hiyo, timu ambazo hazishiriki Ligi Kuu ya Vodacom msimu wa 2016/2017 zitaanza kutangaza wachezaji walioachwa kuanzia Juni 15, 2016 hadi Juni 30, mwaka huu.
    Jeremiah Juma wa Prisons anatakiwa na zote Azam FC na Simba

    Kwa upande wa timu zitakazoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom (VPL), watatumia kipindi cha Juni 15, 2016 hadi Juni 30, 2016 kutangaza usitishwaji mkataba wa wacheaji. Usajili wa utaanza Juni 15 hadi Agosti 6, kwa timu zinazoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
    Pingamizi itakuwa ni Agosti 7 hadi 14, 2016 kabla ya kuthibitisha usajili kwa hatua ya kwanza kati ya Agosti 15 na Agosti 19, 2016 wakati usajili hatua ya pili utaanza Agosti 17, 2016 hadi Septemba 7, 2016 na kitafuatiwa kipindi cha kipindi cha pingamzi hatua ya pili kuanzia Septemba 8 hadi Septemba 14, 2016.
    Septemba 15 hadi Septemba 17, 2016 itakuwa ni kipindi cha kuthibitisha usajili hatua ya pili. 
    Ratiba hiyo inasema kwamba timu zinatakiwa kuandaliwa kuanzi Juni 15 2016 hadi Julai 15, 2016 ambako kuanzia Julai 16, 2016 hadi Agosti 14 ni kipindi cha mechi za kirafiki za ndani na nje. Ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara itatoka kati ya Julai 16 hadi Agosti 14.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: PAZIA LA USAJILI LIGI KUU LAFUNGULIWA WIKI IJAYO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top