• HABARI MPYA

    Friday, June 17, 2016

    PACHA WA NGOMA ZIMBABWE AJA LEO KUSAINI YANGA

    KIUNGO mshambuliaji wa kimataifa wa Zambia, Obrey Chirwa (pichani kulia) anatarajiwa kuwasili leo Dar es Salaam kukamilisha usajili wake kujiunga na Yanga SC.
    Chirwa alikuwa mshambuliaji pacha wa Donald Ngoma katika klabu ya FC Platinums ya Zimbabwe.
    Na baada ya Ngoma kuhamia Yanga, akawashauri viongozi wa timu hiyo wamchukue winga huyo wa kulia wa timu ya vijana ya Zambia chini ya umri wa miaka 23.   
    Na inaaminika Yanga imekubali kutoa zaidi ya dola za Kimarekani 100 000 kuipata saini ya Chirwa ambaye anatokea FC Platinum ya Zimbabwe, klabu waliyotokea wachezaji wake wengine, Wazimbabwe Thabani Kamsuoko na Ngoma.
    Mwaka jana, Chirwa alikataa kujiunga na Hobro IK ya Denmark kwa kutoridhishwa  na malipo - na maana yake Yanga itakuwa imempa mshahara mzuri.
    Yanga inataraka kutuma jina la mchezaji huyo Shirikisho la Soka Afrika (CAF) ili awahi kucheza mechi za Kundi A Kombe la Shirikisho.
    Na mpango huo utafanywa mapema tu atakapokamilisha usajili wake leo akiwasili. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: PACHA WA NGOMA ZIMBABWE AJA LEO KUSAINI YANGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top