• HABARI MPYA

  Sunday, June 19, 2016

  MAZEMBE YAANZA VYEMA, YAIPIGA 3-1 MEDEAMA, KALABA AFUNGA MAWILI

  TP Mazembe imeanza kwa kishindo hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika, baada ya kuibamiza Medeama ya Ghana mabao 3-1 jioni ya leo Uwanja wa Mazembe mjini Lubumbashi.
  Katika mchezo huo wa Kundi lenye timu za MO Bejaia na Yanga pia zitakazomenyana leo baadaye nchini Algeria, hadi mapumziko, Mazembe walikuwa mbele kwa mabao 2-1.
  Wageni walianza kwa bao la Akowuah dakika ya pili, kabla ya Rainford Kalaba kuisawazishia Mazembe dakika ya 15 na Coulibaly kufunga la pili dakika ya 45.
  Rainford Kalaba amefunga mabao mawili, TP Mazembe ikishinda 3-1

  Kalaba akawainua tena vitini mashabiki wa nyumbani, Uwanja wa Tout Puissant Mazembe kwa kufunga bao la tatu dakika ya 69.
  Mchezo ujao Mazembe itasafiri hadi Tanzania kuwafuata Yanga, wakati Medeama watarudi nyumbani kuisubiri MO Bejaia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAZEMBE YAANZA VYEMA, YAIPIGA 3-1 MEDEAMA, KALABA AFUNGA MAWILI Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top