• HABARI MPYA

  Saturday, June 04, 2016

  MARAIS WOTE HAWA WA TFF, MMOJA TU ALITUPELEKA AFCON

  Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye (katikati) akiwa na Marais wa vipindi tofauti wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), tangu za FAT (Chama cha Soka Tanzania) jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kabla ya mchezo wa Taifa Stars na Misri ambao wenyeji wamefungwa 2-0. Kutoka kulia ni Said El Maamry, Jamal Malinzi, Muhiddin Ndolanga na Leodegar Tenga. Ni wakati wa El Maamry tu Taifa Stars ilifuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 1980, lakini baada ya hapo amefuatiwa na Mohammed Mussa (sasa marehemu) Ndolanga, Tenga na Malinzi (wa sasa) na wote hawajafanikiwa kuvunja rekodi hiyo. Je, Malinzi atafanikiwa kabla ya kuondoka madarakani?  

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MARAIS WOTE HAWA WA TFF, MMOJA TU ALITUPELEKA AFCON Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top