• HABARI MPYA

  Monday, June 06, 2016

  KILA KLABU LIGI KUU YATAKIWA LAZIMA IWE NA UWANJA WAKE KUANZIA MSIMU UJAO

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KLABU za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara zimetakiwa kuanzia msimu ujao ziwe na ofisi, Uwanja wa mazoezi, kuendeleza programu za vijana ikiwa ni pamoja na kuwapa haki ya kusoma.
  Hayo yamefikiwa katika kikao cha Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Jumapili (Juni 05, 2016) cha kupitia taarifa mbalimbali za ligi na kukubaliana namna ya kuboresha mashindano mbalimbali ikiwamo Ligi Kuu, Kombe la Shirikisho la Azam (ASFC), Ligi Daraja la Kwanza ya Startimes, Ligi Daraja la Pili na Ligi ya Mabingwa wa Mkoa kilichofanyika mjini Dar es Salaam.
  Rais wa TFF, Jama Malinzi aliongoza kikao cha Kamati ya Utendaji 

  "Kadhalika kamati iliangalia uendeshaji wa Ligi za vijana wenye umri wa chini ya miaka 20 na Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania (TWPL) ambayo wiki iliyopita ilipata udhamini wa haki za kuonyeshwa kwenye televisheni kutoka kituo cha televisheni cha Azam," imesema taarifa ya TFF.
  Aidha, Kamati ya Utendaji imepitisha azimio la kanuni ya leseni ya klabu kuwa ni lazima ianze kutumika msimu mpya wa mashindano wa 2016/17.
  Mahitaji ya kanuni hiyo ni pamoja na klabu kuwa na Watendaji wa kuajiriwa kama vile Katibu Mkuu (GS), Mkurugenzi wa Ufundi (TD), Ofisa Usalama (Security Officer) na taarifa ya fedha zilizokaguliwa pamoja na Meneja wa Fedha ambaye atakuwa na uwezo wa kuandaa taarifa za fedha zitakazokaguliwa na wakaguzi wa mahesabu.
  "Pia klabu zinatakiwa kuwa na ofisi, Uwanja wa mazoezi, kuendeleza program ya vijana ikiwa ni pamoja na kuwapa haki ya kusoma na  na kwamba hakuna mmiliki mmoja anayeruhusiwa kuwa na timu zaidi ya moja katika ligi," imesema taarifa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KILA KLABU LIGI KUU YATAKIWA LAZIMA IWE NA UWANJA WAKE KUANZIA MSIMU UJAO Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top