• HABARI MPYA

  Monday, June 06, 2016

  IBRAHIMOVIC AWAAMBIA MAN UNITED; "JUMANNE MTASIKIA HABARI NZURI, MTAFURAHI"

  MSHAMBULIAJI aliyemaliza Mkataba wake PSG ya Ufaransa, Zlatan Ibrahimovic amewaweka 'mkao wa kula' mashabiki wa Manchester United Jumapili baada ya kuwaambia kutakuwa na 'tangazo kubwa' Jumanne.
  Mshambuliaji huyo anatarajiwa kusaini Mkataba wa mwaka mmoja Old Trafford wiki hii kuelekea michuano ya Kombe la Mataifa ya Ulaya nchini Ufaransa.
  Ibrahimovic - aliyeanza katika kikosi cha Sweden kilichoshinda 3-0 dhidi ya Wales - atatuma muda wa nje ya kambi ya timu yake ya taifa na kocha Erik Hamren wiki hii kwa ajili ya masuala yake binafsi.

  Zlatan Ibrahimovic akiichezea Sweden dhidi ya Wales jana katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa   PICHA ZAIDI GONGA HAPA  

  ZLATAN IBRAHIMOVIC MSIMU ULIOPITA

  Mechi alizocheza: 31
  Mabao aliyofunga: 38
  Pasi za mabao: 13
  Nafasi alizotengeneza: 45
  Mashuti sawia: Asilimia 60
  *Takwimu hizi ni kwa Ligue 1  
  Mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 34 anatarajiwa kuzindua nembo mpya ya mavazi kesho, lakini pia inatarajiwa atazungumzia na uhamisho wake Man United.
  Habari zozote kuhusu uhamisho wake sambamba na uzinduzi wa nembo ya mavazi zitaleta msisimko mkubwa, huku Ibrahimovic ikifikiriwa amepewa ofa ya mshahara wa Pauni 200,000 kwa wiki.
  "Kutakuwa na tangazo kubwa Juni 7. Litakuwa bomu kubwa la majira haya ya joto ya usajili,"amesema Ibrahimovic akizungumza na Televisheni ya Sweden.
  "Imekaa poa, ikoa poa zaidi ya vizuri. Mengi yatatatokea na habari hizi, hivyo ni matumaini utafurahi," amesema.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: IBRAHIMOVIC AWAAMBIA MAN UNITED; "JUMANNE MTASIKIA HABARI NZURI, MTAFURAHI" Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top