• HABARI MPYA

    Friday, June 17, 2016

    CHIRWA TAYARI YUKO DAR ES SALAAM KUSAINI MKATABA WA MIAKA MIWILI YANGA

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    KIUNGO mshambuliaji wa kimataifa wa Zambia, Obrey Chirwa amewasili jioni ya leo Dar es Salaam tayari kukamilisha usajili wake kujiunga na Yanga SC.
    Chirwa alikuwa mshambuliaji pacha wa Donald Ngoma katika klabu ya FC Platinums ya Zimbabwe.
    "Amewasili muda huu, ndiyo nimempokea, tunakwenda kumalizana naye sasa,"amesema Kaimu Katibu wa Yanga, Baraka Deusdedit akizungumza na BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE.
    Na baada ya Ngoma kuhamia Yanga, akawashauri viongozi wa timu hiyo wamchukue winga huyo wa kulia wa timu ya vijana ya Zambia chini ya umri wa miaka 23.  
    Obrey Chirwa akiwa kwenye gari la Katibu wa Yanga, Baraka Deusdedit baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam wakielekea makao makuu ya klabu, ambako anatarajiwa kusaini Mkataba wa miaka miwili 

    Na inaaminika Yanga imekubali kutoa zaidi ya dola za Kimarekani 100 000 kuipata saini ya Chirwa ambaye anatokea FC Platinum ya Zimbabwe, klabu waliyotokea wachezaji wake wengine, Wazimbabwe Thabani Kamsuoko na Ngoma.
    Mwaka jana, Chirwa alikataa kujiunga na Hobro IK ya Denmark kwa kutoridhishwa  na malipo - na maana yake Yanga itakuwa imempa mshahara mzuri.
    Obrey Chirwa akifurahia moja ya mabao yake aliyofunga Platinums FC ya Zimbabwe

    Yanga inataraka kutuma jina la mchezaji huyo Shirikisho la Soka Afrika (CAF) ili awahi kucheza mechi za Kundi A Kombe la Shirikisho.
    Na mpango huo utafanywa mapema tu atakapokamilisha usajili wake leo akiwasili. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: CHIRWA TAYARI YUKO DAR ES SALAAM KUSAINI MKATABA WA MIAKA MIWILI YANGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top