• HABARI MPYA

  Tuesday, June 07, 2016

  BOUBACAR ATUPIWA VIRAGO YANGA, MBUYU TWITE ASAINI MKATABA MPYA

  Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM
  BEKI Mkongomani anayeweza kucheza nafasi za kiungo pia, Mbuyu Junior Twite ameongeza Mkataba wa miaka miwili kuendelea kuichezea Yanga, lakini kiungo kutoka Niger Issoufou Boubacar Garba amepewa barua ya kuvunjiwa Mkataba.
  Habari ambazo BIN ZUBEIRY SPORTS – ONLINE imezipata kutoka Yanga SC, jioni hii zinasema kwamba Mbuyu amesaini leo saa chache baada ya Garba kupewa barua yake ‘send off’.
  Mbuyu Twite (kulia) akitia dole gumba kwenye fomu za Yanga huku akishuhudiwa na Meneja Masoko, Omar Kaaya (kushoto)

  Na Garba ameambiwa tu anaachwa kwa sababu ya kushindwa kuwa katika kiwango kinachohitajika kwa matumizi ya timu, wakati Mbuyu kwa mara nyingine anavuna matunda ya jitihada zake uwanjani.
  Garba alisajiliwa Yanga SC Desemba mwaka jana baada ya majaribio ya siku mbili tu, lakini tangu hapo amecheza mechi 11 tu na kufunga mabao matatu likiwemo lile la katika sare ya 1-1 na Al Ahly ya Misri mjini Dar es Salaam katika Ligi ya Mabingwa Afrika miezi miwili iliyopita.
  Kabla ya Yanga, Garba amewahi kuchezea 
  AS FAN na AS Douanes  za kwao Niger, Muangthong United na Phuket za Thailand, Club Africain na ES Hammam-Sousse za Tunisia.
  Mbuyu Twite aliyesajiliwa Yanga SC miaka minne iliyopita kutoka APR ya Rwanda, katika kipindi chote amecheza mechi 135 na kufunga mabao manne.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BOUBACAR ATUPIWA VIRAGO YANGA, MBUYU TWITE ASAINI MKATABA MPYA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top