• HABARI MPYA

  Tuesday, June 07, 2016

  BEKI BORA LA LIGA ATUA MAN UNITED KWA VIPIMO

  BEKI Eric Bailly anatarajiwa kufanyiwa vipimo leo Manchester United katika mpango wa kusajiliwa kwa dau la Pauni Milioni 30 kutoka Villarreal.
  Klabu hizo zimekwishakubaliana dau la mchezaji huyo wa kimataifa wa Ivory Coast mwenye umri wa miaka 22 na amewasili mjini Manchester kukamilisha uhamisho wake na wawakilishi wake wanatarajiwa kuwa wamemaliza dili hilo hadi kufika Ijumaa.
  Bailly ambaye ni miongoni mwa mabeki bora Hispania kwa sasa, atakuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na kocha mpya, Mreno Jose Mourinho Manchester.

  Manchester United inamtaka beki wa Villarreal, Eric Bailly PICHA ZAIDI GONGA HAPA 
  Villarreal iko tayari kumuuza United mchezaji huyo iliyemnunua kutoka kwa wapinzani wa La Liga, Villarreal Janaury 2015 kwa matarajio ya kupata faida ya Pauni Milioni 4.4.
  Mbali na Bailly, anayewaniwa pia na Bayern Munich, Barcelona, Paris Saint-Germain, Arsenal na Manchester City, Mourinho pia anataka kuimarisha kikosi Man United kuwa kuwasajili Zlatan Ibrahimovic aliyemaliza Mkataba PSG na Nemanja Matic wa Chelsea.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BEKI BORA LA LIGA ATUA MAN UNITED KWA VIPIMO Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top