• HABARI MPYA

    Saturday, May 07, 2016

    YANGA NA SAGRADA ESPERANCA KATIKA PICHA LEO

    Winga wa Yanga, Godfrey Mwashiuya akivuta mguu kupiga krosi baada ya kumzidi kasi beki wa Sagrada Esperanca ya Angola katika mchezo wa kwanza wa mchujo wa kuwania kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika uliofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jioni ya leo. Yanga imeshinda 2-0

    Mshambuliaji wa Yanga, Amissi Tambwe akivuta mguu kupiga shuti mbele ya mebeki wa Sagrada Esperanca 

    Beki wa Yanga, Juma Abdul akipitisha mguu katikati ya miguu ya mchezaji wa Sagrada Esperanca kuondosha mpira

    Kipa wa Sagrada Esperanca akidaka mpira wa juu dhidi ya wachezaji wa Yanga, huku akilindwa na mabeki wake

    Kiungo wa Yanga, Haruna Niyonzima akiambaa na mpira pembeni ya mchezaji wa Sagrada Esperanca

    Mashabiki wa Yanga kwa raha zao leo Uwanja wa Taifa

    Simon Msuva akishagilia kibabe mbele ya jukwaa la mashabiki wa Simba baada ya kuifungia Yanga bao la kwanza

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA NA SAGRADA ESPERANCA KATIKA PICHA LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top