• HABARI MPYA

    Wednesday, May 18, 2016

    YANGA NA AZAM FAINALI KOMBE LA ASFC SASA WIKI IJAYO TAIFA

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    FAINALI ya kuwania Kombe la Shirikisho Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) itakayozikutanisha Yanga na Azam FC, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam sasa itafanyika Mei 25, 2016.
    Awali fainali hiyo ilipangwa kufanyika Juni 11, 2016 ili kuzipa muda wa kuajindaa timu hizo za Dar es Salaam mara baada ya michezo ya mwisho ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara Mei 22, mwaka huu.
    Lakini imerudishwa nyuma ili iwe ndani ya kalenda ya msimu ya TFF, ambayo inafikia tamati Mei 31, mwaka huu.
    Aidha, tarehe ya awali ilipangwa kutokana ratiba kubana hasa ya timu ya soka ya Tanzania ‘Taifa Stars’ ambayo ina mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Kenya ‘Harambee Stars’ unaotarajiwa kufanyika Mei 29, mwaka huu. Mchezo huo unaingia kwenye kalenda ya FIFA.

    Taifa Stars itacheza mechi hiyo ikiwa ni maandalizi ya mchezo wake dhidi ya Misri unaotarajiwa kufanyika Juni 4, 2016 jijini Dar es Salaam kuwania kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON).
    Tayari TFF imefafanua iwapo Bingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwa msimu 2015/16 inayoendelea atashinda pia taji katika fainali za Kombe la Shirikisho la ASFC, ndiye atayeiwakilisha nchi katika michuano ya Ligi ya mabingwa wa Afrika msimu wa 2016/17.
    Kwa msingi huo, timu itakayofungwa katika fainali ya Kombe ASFC linalodhaminiwa na kituo cha Televisheni cha Azam, ndiyo itakayowakilisha nchi kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika katika msimu wa 2016/17
    Fainali ya Kombe la Shirikisho inakuja baada ya mchuano iliyoshindanisha timu 64 za Ligi Kuu Tanzania Bara - VPL (16); Ligi Daraja la Kwanza -FDL (24), Ligi Daraja la Pili – SDL (24) 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA NA AZAM FAINALI KOMBE LA ASFC SASA WIKI IJAYO TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top