• HABARI MPYA

    Friday, May 06, 2016

    YANGA KUWAVAA WAANGOLA KESHO BILA KAMUSOKO NA NGOMA

    Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
    YANGA SC kesho itawakosa wachezaji wake tegemeo wa kimataifa wa Zimbabwe, kiungo Thabani Scara Kamusoko na mshambuliaji Donado Dombo Ngoma katika mechi ya kwanza ya mchujo wa kuwania kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Sagrada Esperanca ya Angola Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
    Ofisa Habari wa Yanga, Jerry Muro amesema wawili hao kesho watakuwa wanatumikia adhabu ya kadi za njano mfululizo walizopewa katika mechi dhidi ya Al Ahly mwezi uliopita.
    Hata hivyo, Muro amesema Yanga haitaathirika kwa kuwakosa wawili hao wenye mchango mkubwa katika mafanikio ya timu msimu huum, kwani kocha Mholanzi amekwishawaandaa wachezaji wengine wa kuziba nafasi zao.
    Yanga itakosa huduma ya Thabani Kamusoko kesho dhidi ya Sagrada Esperanca

    Muro apia ametaja viingilio vya mchezo huo, ambavyo ni Sh. 5,000 kwa viti vya rangi ya chungwa, wakati viti vya bluu na kijani watu wataketi kwa Sh. 7,000, VIP B na C watu wataketi kwa Sh 20,000 na VIP na VIP A  itakuwa Sh.30,000.
    Sagrada Esperanca waliwasilia usiku wa kuamkia leo na kufikia katika hoteli ya Protea na jioni ya leo itafanya mazoezi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. 
    Mchezo huo utachezeshwa na marefa kutoka, Joseph Odartei Lamptey atakayepuliza filimbi akisaidiwa na washika vibendera David Laryea na Malik Alidu Salifu, wakati Kamisaa ni Asfaw Luleseged Begashaw kutoka Ethiopia.
    Mchezo wa marudiano utachezeshwa na marefa wa Madagascar Mei 17, mwaka huu Uwanja wa Sagrada Esperanca, zamani Quintalao do Dundo na utachezweshwa .
    Hao ni Hamada el Moussa Nampiandraza atakayepuliza filimbi, akisaidiwa na washika vibendera Velomanana Ferdinand Jinoro na Jean Thierry Djaonirina.
    Yanga imeangukia katika kapu la kuwania kucheza hatua ya makundi ya Shirikisho, baada ya kutolewa na Al Ahly ya Misri katika hatua ya 16 Bora ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa jumla ya mabao 3-2, ikilazimishwa sare ya 1-1 Dar es Salaam na kufungwa 2-1 Alexandria.
    Yanga ilianza vizuri tu kwa kuzitoa Cercle de Joachim ya Mauritius kwa jumla ya mabao 3-0, ikishinda 1-0 ugenini na 2-0 nyumbani kabla ya kuitoa na APR ya Rwanda kwa jumla ya mabao 3-2, ikishinda 2-1 Kigali na kutoa sare ya 1-1 Dar es Salaam.
    Kwa upande wao, Sagrada Esperanca katika Raundi ya Awali waliitoa Ajax Cape Town ya Afrika Kusini kwa jumla ya mabao 3-2 baada ya kufungwa 2-1 ugenini na kushinda 2-0 nyumbani. Katika Raundi ya kwanza wakaitoa LD Maputo ya Msumbiji kwa jumla ya mabao 2-1 ikishinda 1-0 nyumbani na kutoa sare ya 1-1 ugenini na kwenda hatua ya 16 Bora, ambako waliitoa V. Club Mokanda ya Kongo kwa jumla ya mabao 4-1 wakishinda 2-1 ugenini na 2-0 nyumbani.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA KUWAVAA WAANGOLA KESHO BILA KAMUSOKO NA NGOMA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top