• HABARI MPYA

  Friday, May 06, 2016

  MAZEMBE WAJARIBU BAHATI KOMBE LA SHIRIKISHO MBELE YA WATUNISIA

  BAADA ya kuvuliwa taji la Ligi ya Mabingwa, TP Mazembe ya DRC kesho itacheza mechi ya kwanza ya mchujo wa kuwania kucheza hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika, itakapowakaribisha Stade Gabesien ya Tunisia Uwanja wa Mazembe mjini Lubumbashi.
  Mazembe yenye mshambuliaji Mtanzania, Thomas Emmanuel Ulimwengu iliangukia kwenye kapu la kuwania kucheza Kombe la Shirikisho baada ya kutolewa na Wydad Casablanca kwa jumla ya mabao 3-1, wakifungwa 2-0 Morocco na kulazimishwa sare ya 1-1 Lubumbashi.
  Thomas Ulimwengu sasa ana jukumu la kuibeba TP Mazembe michuano ya Afrika
  Mechi nyingine za kesho ni kati ya Mamelodi Sundowns watakaoikaribisha Medeama ya Ghana,
  Mouloudia Olympique de Bejaia ya Algeria itakayoikaribisha Esperance ya Tunisia na El Merreikh ya Sudan itakayoikaribisha Kawkab Marrakech ya Morocco. 
  Ahli Tripoli ya Libya watakuwa wenyeji wa  Misr Makkassa ya Misri, Etoile du Sahel ya Tunisia wataikaribisha C.F. Mounana ya Gabon, Stade Malien ya Mali watakuwa wenyeji wa FUS Rabat ya Morocco na Yanga SC ya Tanzania Sagrada Esperanca ya Angola.
  Mechi za marudiano zitachezwa wiki ijayo na timu nane zitakazoshinda baada ya matokeo ya jumla zitapangwa katika kundi mawoli ya timu nne kila moja kwa ajili ya kucheza Ligi Ndogo ya michuano.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAZEMBE WAJARIBU BAHATI KOMBE LA SHIRIKISHO MBELE YA WATUNISIA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top