• HABARI MPYA

  Sunday, May 01, 2016

  TIMU PEKEE ISIYO YA LIGI KUU KUWAHI KUCHEZA MICHUANO YA AFRIKA

  Kikosi cha Tanzania Stars ambacho kilikuwa hakishiriki ligi yoyote nchini, kabla ya mchezo wa Kombe la Washindi Afrika (sasa limeunganishwa na Kombe la CAF na kuwa Kombe la Shirikisho) dhidi ya Simba FC ya Uganda Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam mwaka 1999. Timu hizo zilitoka sare ya 1-1 na Tanzania Stars kutolewa kwa jumla ya mabao 3-2 baada ya awali kufungwa 2-1 mjini Kampala, Uganda. Kutoka kulia waliosimama ni Abdallah Msamba (marehemu), Alex Kajumulo, Twaha Hamidu na Sanifu Lazaro. Katikati kutoka kulia ni Zubery Katwila, Yussuf Macho, Mohammed Abubakar ‘Phantom’ na Issa Manofu na mbele kutoka kulia ni Thabit Bushako, George Masatu, Muhehe Kihwelo (marehemu), William Fahnbulllar na Malota Soma ‘Ball Jaggler’.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TIMU PEKEE ISIYO YA LIGI KUU KUWAHI KUCHEZA MICHUANO YA AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top