• HABARI MPYA

  Friday, May 13, 2016

  TERRY APEWA MKATABA MPYA WA MWAKA MMOJA CHELSEA

  CHELSEA imempa ofa ya Mkataba mpya wa mwaka mmoja, Nahodha wake, John Terry na sasa ni juu yake kubaki au kuondoka Stamford Bridge msimu ujao.
  Terry na wakala wake agent, Paul Nicholls, wamekutana na Mkurugenzi wa Chelsea, Marina Granovskaia na Mwenyekiti, Bruce Buck kwa mazungumzo katika viwanja vyao vya mazoezi vya Cobham wiki hii.
  Klabu hiyo imethibitisha leo kwamba Terry anaweza kubakia baada ya Juni 30, wakati Mkataba wake utakapomalizika, ingawa Chelsea imemuachia mkongwe huyo wa umri wa miaka 35 kuamua.
  Nahodha wa Chelsea, John Terry amepewa ofa ya Mkataba mpya wa mwaka mmoja abaki msimu ujao PICHA ZAIDI GONGA HAPA

  WASIFU WA JOHN TERRY: 

  Kuzaliwa: Desemba 7, 1980
  Umri: Miaka 35
  Klabu pekee aliyochezea: Chelsea
  Jumla ya mechi: 703
  Mataji aliyoshinda: Ligi Kuu (2005, 2006, 2010, 2015), FA Cup (2000, 2007, 2009, 2010, 2012), Kombe la Ligi (2005, 2007, 2015), Ligi ya Mabingwa (2012), Europa League (2013)
  Mechi za kimataifa (England): 78 
  Msemaji wa klabu amesema; "Marina Granovskaia na Bruce Buck wamekutana na John na wakala wake na kumpa ya Mkataba wa mwaka mmoja abaki,".
  "Na wakati msimu unaelekea ukingoni, haya ni maamuzi mazito kwa John na familia yake na kitu ambacho wanakifikiria kwa sasa,".
  Mashabiki wa Chelsea walikuwa wakimpigia debe Nahodha huyo usiku wa Jumatano Uwanja wa Anfield wakitaka Terry aongezewe Mkataba mpya huku wakiwa wamebeba mabango yanayoonyesha mataji mengi ambayo klabu ilishinda chini ya uongozi wake.
  Pamoja na kwamba umri umeenda na kiwango kimeshuka, lakini Terry bado ni kipenzi cha mashabiki wa Stamford Bridge haswa wanapokumbuka mchango wake enzi zake. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: TERRY APEWA MKATABA MPYA WA MWAKA MMOJA CHELSEA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top