• HABARI MPYA

  Tuesday, May 17, 2016

  SERENGETI BOYS YAWALISHA PILIPILI KICHAA WAHINDI, YAWATANDIKA 3-1, MAZIKU APIGA MBILI

  Na Mwandishi Wetu, GOA
  TIMU ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ya Tanzania, Serengeti Boys imeshinda mechi ya kwanza katika michuano ya kirafiki ya vijana Uwanja wa Tilak Maidan, Vasco, Goa, India leo baada ya kuwafunga wenyeji, india mabao 3-1.
  Mabao ya Serengeti Boys yamefungwa na Maziku Amani dakika ya 20 na 28 na Asad Ali dakika ya 47, wakati la india lilifungwa na Komal Thatal dakika ya 36.
  Mchezo wa kwanza, Serengeti Boys ilitoa ya sare kufungana bao 1-1 na Marekani.
  Kikosi kilichoanza Serengeti Boys ikiibugiza 3-1 India


  Michuano hiyo inayoandaliwa na Shirikisho la Soka India (AIFF) ili kuipa mazoezi timu yake kwa ajili ya Fainali za Kombe la Dunia kwa Vijana mwaka 2017 ambazo watakuwa wenyeji.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SERENGETI BOYS YAWALISHA PILIPILI KICHAA WAHINDI, YAWATANDIKA 3-1, MAZIKU APIGA MBILI Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top