• HABARI MPYA

  Sunday, May 01, 2016

  SAMATTA ALIMWA YA NJANO GENK IKICHEZEA 3-1 UBELGIJI

  Na Mwandishi Wetu, BRUGGE
  MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta amelimwa kadi ya njano timu yake KRC Genk ikifungwa mabao 3-1 na Club Brugge katika mchezo wa mchujo wa Ligi Kuu ya Ubelgiji kuwania kucheza michuano ya Ulaya.
  Mchezo huo wa ugenini uliofanyika Uwanja wa Jan Breydelstadion mjini Brugge, Samatta alilimwa kadi hiyo dakika ya 76, ambayo inakuwa ya pili tangu ajiunge na timu hiyo Januari mwaka huu akitokea TP Mazembe ya DRC.
  Mbwana Samatta leo amelimwa kadi ya pili ya njano tangu aanze kucheza Ubelgiji 
  Katika mchezo huo, kwa mara ya kwanza Samatta alicheza dakika zote 90 jahazi la timu yake likizama kwa mabao ya Waholanzi beki Stefano Denswil dakika ya 21, kiungo Ruud Vormer dakika ya 43 na kiungo Myahudi, Lior Refaelov dakika ya 60.
  Bao pekee la Genk leo limefungwa na mshambuliaji Mgiriki, Nikolaos Karelis dakika ya 89.
  Samatta leo amecheza mechi ya 12 tangu ajiunge na Genk akitoka kushinda taji la Ligi ya Mabingwa Afrika na TP Mazembe pamoja na kutwaa tuzo ya Mwanasoka Bora Anayecheza Afrika.
  Katike mechi hizo, ambazo tano tu alianza, mshambuliaji huyo wa zamani wa Simba SC ya Dar es Salaam, amefunga mabao nne, moja katika kila mechi Genk ikishindia 2-1 ugenini dhidi ya wenyeji SV Zulte-Waregem, 4-0 na 4-1 dhidi ya KV Oostende na 3-2 dhidi ya Club Brugge mchezo wa kwanza.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SAMATTA ALIMWA YA NJANO GENK IKICHEZEA 3-1 UBELGIJI Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top