• HABARI MPYA

  Tuesday, May 17, 2016

  RASHFORD AITWA KIKOSI CHA AWALI ENGLAND EURO 2016 UFARANSA

  MSHAMBULIAJI kinda wa Manchester United, Marcus Rashford nyota yake imeendelea kung'ara baada ya kuitwa katika kikosi ncha awali cha England cha wachezaji 26 kwa ajili ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Ulaya,  Euro 2016.
  Kinda huyo wa umri wa miaka 18, Rashford, ambaye alichezea kikosi cha kwanza cha Man United Februari mwaka huu, ni kati ya washambuliaji watano walioitwa na kocha Roy Hodgson jana.
  England itacheza mechi za kirafiki za kimataifa dhidi ya Uturuki, Australia na Ureno kabla ya kwenda Ufaransa kwenye Euro.
  Winga Andros Townsend naye ameitwa baada ya kumalizia vizuri Ligi Kuu ya England akiwa na Newcastle United iliyoteremka daraja.
  Mshambuliaji chipukiiz wa Manchester United, Marcus Rashford amejumuishwa kwenye kikosi cha awali cha England kwa ajili ya Euro 2016

  KIKOSI CHA AWALI CHA WACHEZAJI 26 WA ENGLAND EURO 2016...

  Makipa: Fraser Forster (Southampton), Joe Hart (Manchester City), Tom Heaton (Burnley)
  Mabeki: Ryan Bertrand (Southampton), Gary Cahill (Chelsea), Nathaniel Clyne (Liverpool), Danny Rose (Tottenham), Chris Smalling (Manchester United), John Stones (Everton), Kyle Walker (Tottenham)
  Viungo: Dele Alli (Tottenham), Ross Barkley (Everton), Fabian Delph (Manchester City), Eric Dier (Tottenham), Danny Drinkwater (Leicester City), Jordan Henderson (Liverpool), Adam Lallana (Liverpool), James Milner (Liverpool), Raheem Sterling (Manchester City), Andros Townsend (Newcastle), Jack Wilshere (Arsenal)
  Washambuliaji: Harry Kane (Tottenham), Marcus Rashford (Manchester United), Wayne Rooney (Manchester United), Daniel Sturridge (Liverpool), Jamie Vardy (Leicester City)
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: RASHFORD AITWA KIKOSI CHA AWALI ENGLAND EURO 2016 UFARANSA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top