• HABARI MPYA

    Saturday, May 07, 2016

    PLUIJM AWAANZISHA PAMOJA BUSUNGU NA TAMBWE DHIDI YA WAANGOLA

    Malimi Busungu anaanza na Tambwe leo
    Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
    KOCHA wa Yanga, Mholanzi Hans van der Pluijm amewaanzisha pamoja washambuliaji Malimi Busungu na Amissi Tambwe kwa ajili ya mchezo wa kwanza wa mchujo wa kuwania kuingia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika dhidi ya Sagrada Esperanca ya Angola jioni ya leo. 
    Mchezo huo utaanza Saa 10:00 jioni na utachezeshwa na marefa kutoka Ghana, ambao ni Joseph Odartei Lamptey atakayepuliza filimbi akisaidiwa na washika vibendera David Laryea na Malik Alidu Salifu, wakati Kamisaa ni Asfaw Luleseged Begashaw kutoka Ethiopia.
    Busungu anachukua nafasi ya mshambuliaji Mzimbabwe, Donald Ngoma ambaye anatumikia adhabu ya kadi za njano mfululizo alizopewa kwenye mechi dhidi ya Al Ahly mwezi uliopita.
    Salum Telela amechukua nafasi ya Thabani Kamusoko kikosini Yanga leo

    Aidha, kwa kukosekana kwa Mzimbabwe mwingine , kiungo Thabani Kamusoko, Pluijm amewaanziwha viungo Salum Telela na Haruna Niyonzima.
    Deus Kaseke atacheza kama kiungo wa pembeni, ambaye atakuwa na jukumu la kuwa katikati muda wingi, wakati Simon Msuva atacheza wingi ya kulia.
    Safu ya ulinzi ya Yanga itaendelea kuwa chini ya kipa Deo Munishi ‘Dida’, beki wa kulia Juma Abdul, Oscar Joshua kushoto na kati Kevin Yondan na Nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’.  
    Kikosi kamili cha Yanga ni; Deo Munishi ‘Dida’, Juma Abdul, Oscar Joshua, Kevin Yondan, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Salum Telela, Simon Msuva, Haruna Niyonzima, Malimi Busungu, Amissi Tambwe na Deus Kaseke.
    Katika benchi watakuwapo; Ally Mustafa ‘Barthez’, Mbuyu Twite, Vincent Bossou, Mwinyi Hajji, Geoffrey Mwashiuya, Paul Nonga na Matheo Anthony.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: PLUIJM AWAANZISHA PAMOJA BUSUNGU NA TAMBWE DHIDI YA WAANGOLA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top