• HABARI MPYA

  Friday, May 13, 2016

  MKWASA AUMIZA KICHWA KUPATA WAKALI WA KUIBEBA STARS AFCON

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KOCHA Mkuu wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa wiki ijayo atarajiwa kutangaza kikosi cha wachezaji wake wakaokwenda Kenya kwenye mchezo wa kirafiki wa kimataifa utakaofanyika jijini Nairobi, Mei 29, 2016.
  Mkwasa atakutana na Waandishi wa Habari Mei 18, mwaka huu katika ukumbi wa mikutano wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kutaja kikosi. 
  Pamoja na kuutumia mchezo kuwania kupanda katika viwango vya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), Stars pia itautumia mchezo kama sehemu ya maandalizi yake kabla ya kumenyana na Misri katika mchezo wa Kundi G kuwania kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Africa (AFCON) mwakani, utakaofanyika Juni 4, 2016 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Stars inahitaji kuifunga Misri ili kuweka hai matumaini ya kufuzu fainali hizo za Gabon 2017.
  Misri inaongoza kundi hilo lenye timu tatu baada ya Chad kujitoa kwa pointi zake saba, ikifuatiwa na Nigeria yenye pointi mbili, wakati Tanzania ina pointi moja ni ya mwisho kwa sasa.
  Misri itakuwa inacheza mechi yake ya mwisho Juni 2 Dar es Salaam wakati Stars itamaliza Nigeria Septemba 2 mjini Abuja.
  Stars ikishinda mechi zake mbili za mwisho itafikisha pointi saba hivyo kulingana na Misri - na maana yake timu ya kwenda Gabon kutoka Kundi G itatazamwa kwa wastani wa mabao.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MKWASA AUMIZA KICHWA KUPATA WAKALI WA KUIBEBA STARS AFCON Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top