• HABARI MPYA

  Tuesday, May 17, 2016

  MAZEMBE WANA SHUGHULI NZITO LEO TUNISIA

  RATIBA MECHI ZA MARUDIANO MCHUJI WA KUWANIA MAKUNDI KOMBE LA SHIRIKISHO
  Leo; Jumanne Mei 17, 2016
  Esperance (Tunisia) Vs MO Bejaia (Algeria) (0-0)
  Stade Gabesien (Tunisia) Vs TP Mazembe (DRC) (0-1)
  Kesho; Jumatano Mei 18, 2016
  Sagrada Esperanca (Angola) Vs Yanga SC (Tanzania) (0-2)
  FUS Rabat (Morocco) Vs Stade Malien (Mali) (0-0)
  CF Mounana (Gabon) Vs Etoile du Sahel (Tunisia) (0-2)
  Misr Makkassa (Misri) vs Ahly Tripoli (Libya) (0-0)
  Medeama (Ghana) Vs Mamelodi Sundowns (Afrika Kusini) (1-3)
  Kawkab (Morocco) Vs El Merreikh (Sudan) (0-1)
  Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Thomas Ulimwengu leo ana shughuli nzito Tunisia, wakati timu yake, TP Mazembe itakapohitaji kuulinda ushindi mwembamba wa 1-0 dhidi ya Stade Gabasien

  WALIOKUWA mabingwa wa Afrika, TP Mazembe leo wanamenyana na wenyeji Stade Gabesien mjini Tunis katika mchezo wa marudiano wa mchujo wa kuwania kuingia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.
  Katika mchezo wa leo, Mazembe inayomtegemea mshambuliaji Mtanzania, Thomas Ulimwengu itahitaji sare yoyote baada ya awali kushinda 1-0 katika mchezo wa kwanza wiki iliyopita mjini Lubumbashi ili kuingia hatua ya makundi.
  Huo ni mtihani mzito mbele ya Mazembe na haswa ikizingatiwa wanacheza Kaskazini mwa Afrika, tena Tunisia ambako timu zake hujizatiti mno katika michuano ya Afrika hususan zinapocheza nyumbani.
  Ikumbukwe Mazembe iliangukia kwenye kapu hilo la kuwania hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho baada ya kutolewa na Wydad Casablanca ya Morocco kwa jumla ya mabao 3-1, ikifungwa 2-0 ugenini na kulazimishwa sare ya 1-1 Lubumbashi.
  Mazembe ikavuliwa mapema ubingwa wa Afrika na sasa inasaka tiketi ya kuwania ubingwa wa michuano midogo ya CAF.
  Mechi nyingine ya leo ni kati ya wenyeji, Esperance ya Tunisia dhidi ya MO Bejaia ya Algeria ambazo zilitoka sare ya 0-0 katika mchezo wa kwanza. 
  Michuano hiyo itaendelea kesho, wakati Sagrada Esperanca ya Angola watakapoikaribisha Yanga SC ya Tanzania. Yanga ilishinda 2-0 mechi ya kwanza.
  FUS Rabat ya Morocco wataikaribisha Stade Malien ya Mali, baada ya sare ya 0-0 katika mchezo wa kwanza. CF Mounana ya Gabon itajaribu kupindua kipigo cha 2-0 ilichokipata kutoka kwa Etoile du Sahel ya Tunisia katika mchezo wa kwanza.
  Misr Makkassa ya Misri itarudiana na Ahly Tripoli ya Libya baada ya sare ya 0-0 katika mchezo wa kwanza, Medeama ya Ghana itajaribu kukipiku kipigo cha 3-1 katika mchezo wa kwanza ugenini mbele ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, wakati El Merreikh ya Sudan itajaribu kuulinda ushindi wake mwembamba wa 1-0 nyumbani dhidi ya wenyeji Kawkab nchini Morocco leo.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAZEMBE WANA SHUGHULI NZITO LEO TUNISIA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top