• HABARI MPYA

  Friday, May 13, 2016

  'KIJEBA' AIONDOA UGANDA MICHUANO YA U-20 AFRIKA, RWANDA YAPETA MEZANI

  KAMATI ya Maandalizi ya Mashindano chini ya Umri wa miaka 20 ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) imeiondoa Uganda kwenye mbio za kuwania tiketi ya fainali za mwakani za michuano hiyo baada ya kumtumia mchezaji aliyezidi umri dhidi ya Rwanda.
  Mchezo huo ulifanyika Jumamosi ya Aprili 23, 2016 mjini Kampala na Uganda kushinda 2-1 hivyo kufuzu kusonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 3-2 baada ya sare ya 1-1 katika mchezo wa kwanza Kigali.
  Hata hivyo, Shirikisho la Soka Rwanda (FERWAFA) likaikatia rufaa Uganda kwa kuwatumia wachezaji Tumwesigye Frank, Aheebwa James, Lwalirwa Halid na Kizza Martin.
  FERWAFA iliwalalamikia wachezaji hao kuonyesha pasipoti zenye umri tofauti na ule waliosajiliwa na klabu zao, Vipers na SC Villa kwa ajili ya michuano ya Afrika mwaka 2016.
  Baada ya kutazamwa kwa mtandao wa usajili wa CAF (CMS), ikagundulika ni Aheebwa James pekee mwenye umri unaotafutiana upande mmoja, pasipoti yake ikionyesha amezaliwa Mei 19, mwaka 1998 na leseni yake ya kucheza michuano ya klabu Afrika ikionyesha amezaliwa Machi 27, mwaka 1997.
  Kwa matokeo hayo, Rwanda sasa inasonga mbele na itamemyana na Misri katika Raundi ya Pili ya kufuzu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: 'KIJEBA' AIONDOA UGANDA MICHUANO YA U-20 AFRIKA, RWANDA YAPETA MEZANI Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top