• HABARI MPYA

  Tuesday, May 17, 2016

  GOLDEN ARROW YAMTAKA BURE HAJIB BAADA YA KUFUZU MAJARIBIO

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MSHAMBULIAJI wa Simba SC, Ibrahim Hajib amefuzu majaribio katika klabu ya Lamontville Golden Arrows FC ya Ligi Kuu ya ABSA Afrika Kusini.
  Hata hivyo, klabu hiyo haiko tayari kumnunua mchezaji huyo bali inataka kumchukua kama mchezaji huru na kumsainisha Mkataba.
  Kwa sababu hiyo, klabu hiyo imemuambia Hajib arejee Dar es Salaam kuangalia kama Mkataba wake umekwisha apeleke uthibitisho Afrika Kusini ili apewe Mkataba Arros.
  Wakala wa mchezaji huyo, Juma Ndabila ameiambia BIN ZUBEIRY SPORTS – ONLINE kwamba wanarejea leo Dar es Salaam pamoja na Hajib.
  Ibrahim Hajib (kushoto) akiwa na wakala wake, Juma Ndabila

  “Amefuzu majaribio, lakini kuna suala la Mkataba hapa, yeye alisema kamaliza Mkataba, na Simba wanasema bado ana Mkataba, kwa hivyo anarudi kutatua hilo suala,”amesema Ndabila.
  Kwa upande wake, wakala aliyemuunganishia majaribio Hajib Afrika Kusini, Rodgers Mathaba amesema kwamba mchezaji huyo amepewa fursa ya kurudi Arrow wakati wowote akiwa mchezaji huru.
  “Amefuzu majaribio, sasa ni juu yake anatakiwa hapa kama mchezaji huru, anarudi Dar es Salaam kushughulikia Mkataba wake, nafasi yake ipo wazi hapa wakati wowote,”amesema  Mathaba. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: GOLDEN ARROW YAMTAKA BURE HAJIB BAADA YA KUFUZU MAJARIBIO Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top