• HABARI MPYA

    Friday, May 13, 2016

    FATMA NDIYE KATIBU MKUU MPYA WA FIFA

    SHIRIKISHO la Soka la Kimataifa leo limemteua Fatma Samba Diouf Samoura wa Senegal kuwa Katibu Mkuu wake (SG).
    Samoura, mwanamama mwenye uzoefu wa miaka 21 wa kufanya Shirika la Umoja wa Mataifa, ambaye kwa sasa Mratibu Mkazi wa UNDP mchini Nigeria, uteuzi wake umetangazwa na Rais wa FIFA, Mtaliano Gianni Infantino katika Mkutano Mkuu wa 66 wa FIFA mjini Mexico City.
    “Fatma ni mwanamke mwenye uzoefu wa kimataifa ambaye ameshughulikia masuala mazito,” amesema Rais Infantino.

    Fatma Samba Diouf Samoura ndiye Katibu Mkuu mpya wa FIFA


    “Amethibitisha uwezo wa kutengeneza na kuongoza timu, na kuboresha namna utendaji wa oganazesheni. Muhimu kwa FIFA, anafahamu pia uwazi na ushirikishaji ni moyo wa mwenendo wowote mzuri,”.
    Mama Samoura anayezungumza kwa ufasaha lugha za Kifaransa alichozaliwa nacho, Kiingereza, Kispanyola na Kitaliano, ataanza kazi ya Ukatibu Mkuu katikati ya Juni.
    Tangu ameanza kufanya kazi UN kama Ofisa mkubwa wa mradi chakula mjini Rome mwaka 1995, Mama Samoura amekuwa mwakilishi au Mkurugenzi wa mataifa sita; Djibouti, Cameroon, Chad, Guinea, Madagascar and Nigeria. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: FATMA NDIYE KATIBU MKUU MPYA WA FIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top