• HABARI MPYA

    Sunday, May 08, 2016

    EL MERREIKH YAPATA USHINDI MWEMBAMBA NYUMBANI

    TIMU ya El Merreikh ya Sudan jana imepata ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Kawkab Marrakech ya Morocco katika mchezo wa kwanza wa mchujo wa kuwania kufuzu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.
    Sasa Merreikh itatakiwa kwenda kuulinda ushindi huo kiduchu wiki ijayo mjini Marakech, Morocco. 
    Mechi nyingine za jana, Mouloudia Olympique de Bejaia ya Algeria imelazimishwa sare ya bila kufungana na Esperance ya Tunisia sawa na Stade Malien wa Mali waliolazimishwa sare ya 0-0 na FUS Rabat ya Morocco mjini Bamako.
    El Merreikh wamepata ushindi mwembamba jana nyumbani

    Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini imeialza 3-1 Medeama ya Ghana Uwanja wa Lucas Moripe, Yanga SC ya Tanzania ikishinda 2-0 dhidi ya Sagrada Esperanca.
    Juzi zilichezwa mechi mbili, Ahli Tripoli ya Libya ililazimishwa sare ya 0-0 na Misr Makkassa na Etoile du Sahel wakishinda 2-0 dhidi ya C.F. Mounana.
    Mechi za kwanza za mchujo wa kuwania hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho zinahitimishwa leo kwa mchezo kati ya wenyeji, TP Mazembe na Stade Gabesien ya Tunisia.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: EL MERREIKH YAPATA USHINDI MWEMBAMBA NYUMBANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top