• HABARI MPYA

  Thursday, May 12, 2016

  CHINA AHITIMU MAFUNZO YA UKOCHA DARAJA LA JUU UINGEREZA, SASA ANAHAMIA UEFA

  Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
  KIUNGO wa zamani wa kimataifa wa Tanzania, Athumani Abdallah Mchabwa ‘Athumani China’ amehitimu mafunzo ya juu ya ukocha nchini England.
  China aliyewahi kuchezea Yanga na Simba enzi zake kabla ya kwenda Walsall FC ya Uingereza, ameiambia BIN ZUBEIRY SPORTS – ONLINE kwamba hatua hiyo ni nzuri katika harakati zake za kuwa kocha mkubwa.
  Athumani China amehitimu mafunzo ya juu ya ukocha England  “Wiki iliyopita nimekamilisha mafunzo ya pili ya ukocha FA (England) na sasa nasubiri kukabidhiwa vyeti vyangu na hii ni baada ya mwezi Februari kuhitimu mafunzo ya kwanza ya FA,”amesema China.
  Kiungo huyo aliyewahi pia kuchezea Kajumulo WS kwa muda mfupi, amesema kwamba kwa sasa anajipanga kuanza mafunzo ya awali ya ukocha ya Shirikisho la Soka Ulaya (UEFA).
  “Hii yote ni katika kujiongezea ufahamu ambao tayari ninao kwa wingi kuhusu mpira, maana tukilala tunaota mpira, chakula chetu na pumzi zetu ni mpira tu,”amesema.
  “Vyeti wakati mwingine si kitu zaidi
  ya ufahamu wa kiasili, kocha wa timu ya taifa ya Ghana aliifikisha timu robo fainali ya kombe la Dunia huku akiwa hana hata cheti kimoja kama hiki,”ameongeza.
  Kabla ya mafunzo hayo ya Uingereza, China aliwahi pia kusomea ukocha nchini Brazil mwaka 2000.
  Kwa hapa nyumbani Tanzania, China aliwahi kupata mafunzo mbalimbali ya ukocha katika vipindi alivyokuwa anakuja likizo, ikiwemo mwaka juzi.
  Tangu amestaafu soka, China amekuwa akiishi England ambako pia anafanya shughuli zake nyingine nje ya mambo ya soka.

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CHINA AHITIMU MAFUNZO YA UKOCHA DARAJA LA JUU UINGEREZA, SASA ANAHAMIA UEFA Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top