• HABARI MPYA

  Thursday, May 12, 2016

  CAF YAONGEZA KLABU HATUA YA MAKUNDI KUTOKA NANE HADI 16

  SHIRIKISHO la Soka Afrika limeongeza idadi ya timu za kuingia hatua ya makundi ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho kutoka nane za makundi mawili hadi 16 za makundi manne kuanzia mwaka ujao.
  Hayo yamesemwa na Rais wa CAF, Issa Hayatou katika hotuba ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa shirikisho hilo jana Mexico City nchini Mexico.
  Katika mkutano huo uliohudhuriwa na Rais wa FIFA, Gianni Infantino, aliyeongozana na magwiji wa soka, Samuel Eto'o Fils, Luis Figo, Zvonimir Boban, Hayatou alisema mfumo huo utaanza mwakani.

  Rais wa CAF, Issa Hayatou (kulia) akiwa na Rais wa FIFA, Gianni Infantino mjini Mexico City

  Mfumo wa sasa wa makundi mawili ya timu nne kila moja, washindi wawili wa kila kundi hutinga Nusu Fainali na baadaye timu zinazoshinda kukutana fainali.
  Wazi katika mfumo mpya wa makundi manne, kila kundi litatoa timu moja ya kwenda Nusu Fainali.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: CAF YAONGEZA KLABU HATUA YA MAKUNDI KUTOKA NANE HADI 16 Rating: 5 Reviewed By: Bin Zubeiry Sports - Online

  PATA HABARI POPOTE ULIPO. ZIKITUFIKIA ZITAKUFIKIA

  Scroll to Top